NAFASI YA NAIBU KATIBU MKUU – TUCTA KUWA WAZI
Tarehe 25 Januari 2023, Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Nchini, ambapo
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu TUCTA, Ndugu Cornel L. Magembe aliteuliwa na
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Hivyo kufanya nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
kuwa wazi. Aidha, Kikao cha Kamati ya Utendaji kilifanya Uchaguzi mdogo
ambapo Ndugu Saidi S. Wamba alikaimishwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
hadi hapo Baraza Kuu litakapofanya uchaguzi kwa nafasi hiyo kwa mujibu wa
Katiba ya TUCTA.